Kila taifa duniani limeathiriwa na Virusi vya Corona (ugonjwa ujulikanao kama Covid-19). Watu wengi wameogopa na kutaharuki. Wanahitaji kuona upendo, tumaini na huruma za Kristo na kuusikia ukweli huu katika siku hizi ngumu. Wale walioathiriwa na Virusi pia wanahitaji kupata msaada na tegemeo kutoka kwa watu wa Mungu. Ingawa hiki ni kipindi kigumu, kipindi hiki kinatoa fursa ya kushirikisha upendo wa Kristo kwa wale wanaotuzunguka na kuongoza njia ya kuwasaidia wengine. Lakini pia tunahitaji kufahamu namna ya kujitunza sisi wenyewe na wengine kuwa salama na kuwa katika nafasi ya kufahamu ukweli kuhusu virusi. Vile vile tunahitaji kushirikisha ukweli kuhusu virusi ili kuokoa maisha. Kipeperushi cha taarifa hizi kimetengenezwa kwa makusudi haya.

Support our work today

DONATE NOW